Kwaya ya Mtakatifu Gaspar del Bufalo ni kwaya ya Parokia ya Damu Takatifu ya Yesu, Tegeta, iliyoko katika Jimbo Katoliki la Bagamoyo. Kwaya hii ilianzishwa rasmi mwaka 1994, ikiwa na lengo la kumtumikia Mungu kupitia huduma ya muziki wa liturujia na kuinua ibada ndani ya Kanisa.
Kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, kwaya imeendelea kuwa imara, ikitenda kazi kwa mapokeo ya kiroho na kwa bidii. Hadi sasa, kwaya ina jumla ya wanakwaya 80, wakiwemo wanawake 50 na wanaume 30.
Kwaya inashiriki kikamilifu katika shughuli zote za kijimbo, kiparokia na kijamii, ikiwa ni pamoja na huduma za Misa Takatifu, shuguli za kitafita za Kanisa na matamasha ya muziki wa Injili. Pia ni chombo cha malezi ya kiroho kwa wanakwaya wake kupitia mazoezi, mafundisho, na semina mbalimbali.