Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni mojawapo ya kwaya rasmi zinazohudumu katika Parokia ya Mt. Petro, Oysterbay, chini ya Dekenati ya Mt. Petro. Ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na lengo la kuinua ibada na kumtumikia Mungu kupitia muziki mtakatifu wa liturujia.
Kwa zaidi ya miongo mitatu ya huduma, kwaya imeendelea kuwa nguzo ya kiroho na kipaji katika parokia, ikihudumu kwa bidii katika ibada mbalimbali na kushiriki kikamilifu katika matukio ya ndani na nje ya Parokia.