Kwaya hii ilianzishwa rasmi mwaka 2018 ikiwa na dhamira ya kumtumikia Mungu kwa njia ya muziki wa liturujia na kukuza ibada ndani ya Kanisa. Hadi sasa ina wanakwaya 40 wanaohudumu kwa moyo wa hiari na kufuata maadili ya Kanisa.
Misioni:
Kumtumikia Mungu kwa njia ya muziki wa liturujia, kukuza ibada, mshikamano, na utumishi ndani ya Parokia na Kanisa kwa ujumla.
Shughuli na Huduma:
Kwaya ya Mtakatifu Dominic Savio (KMDS) inahudumu kikamilifu katika ibada mbalimbali za Kanisa, ikiwemo Misa za Dominika, Misa za ndoa, Misa za jumuiya, Misa za kumbukumbu na shukrani, pamoja na Misa za mazishi. Aidha, kwaya hushiriki na kuandaa matamasha ya muziki wa injili kama vile Tamasha la Yesu ni Mwema (TYM) na Tamasha la "Vibe la Pasaka" linalofanyika kila Dominika ya Pili ya Pasaka, likiwakutanisha wanakwaya kutoka ndani na nje ya Jimbo. Vilevile, KMDS imefanikiwa kurekodi albamu mbili na nyimbo kadhaa za single, ambazo zimeendelea kuimarisha huduma ya muziki wa liturujia na kuinua kiwango cha ibada katika Parokia.