Kwaya ya Mt. Sesilia ilianzishwa na kusimikwa rasmi mwezi August mwaka 1980 ikiwa na idadi ya wanakwaya 40 chini ya uongozi wa ndugu Melchior Haule. Kwaya ilianzishwa kuhudumia kigango cha Mavurunza ambacho kilikuwa chini ya parokia ya Msewe. Kigango cha Mavurunza hatimaye kilipandishwa hadhi ya kuwa parokia ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili mnamo tarehe 6Januari 2001. Kwaya ya Mt.Sesilia ni miongoni mwa kwaya zinazounda UKWAKATA katika dekania ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu Mavurunza.
Kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake, kwaya ya Mt. Sesilia imekuwa ikishiriki katika uinjilishaji kwa njia ya nyimbo na kuendeleza liturujia ya kanisa katoliki katika ibada mbalimbali. Tangu mwaka 2001 kwaya ya Mt. Sesilia imekuwa ikitoa huduma ya uimbaji kila domnika kwenye ibada ya misa ya 3 inayoanza saa nne kamili asubuhi.
Uongozi katika kwaya ya Mt. Sesilia katika vipindi mbalimbali tangu kuanzishwa kwake katika nafasi ya mwenyekiti ni kama ifuatavyo;
Idadi ya wanakwaya tangu kuanzishwa kwake imekuwa kati ya 40-50.
Kwa kipindi chote cha uhai wake, kwaya ya Mt. Sesilia imefanikiwa kurekodi albamu zifuatazo.
Misioni:
Kumtumikia Mungu na Kanisa Katoliki kupitia nyimbo takatifu, kukuza mshikamano wa kiimani, na kuendeleza sanaa ya muziki wa liturujia kwa ustadi na ibada.
Shughuli na Huduma:
Kwaya huhudumu katika misa za Jumapili na Sikukuu za Kanisa, misa za ndoa, misa za jumuiya ndogo ndogo, na misa za kumbukumbu na shukrani. Pia hufanya mazoezi ya nyimbo mara kwa mara, kushiriki mashindano ya kwaya na matamasha ya kiroho, na kushiriki katika huduma za kijamii na upendo wa jirani.