L O A D I N G


The Catholic Choir Apostolate of Tanzania – Archdiocese of Dar es Salaam. Ukwakata brings together passionate voices and dedicated instructors, empowering choirs to grow musically, spiritually, and as one vibrant community.


Contact Info

Postal Address
P.O Box 90060,
Dar es Salaam, Tanzania

Physical Address
S&F House, Block 30D, Plot No 21, 2nd floor, Mwinjuma Road, Kinondoni

Phone No
+255 222 762 081/0
+255 735 923 521

Email Address
info@ukwakata.or.tz




Contact info

Phone No
+255 222 762 081/0
+255 735 923 521

Email Address
info@ukwakata.or.tz

UKWAKATA ARCHDIOCESE OF DAR ES SALAAM
Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili
Kwaya ya Mt. Sesilia – Mavurunza
Established: 1980
Deanery: Mavurunza
(Mt. Theresia wa Mtoto Yesu)
Parish: Mavurunza
(Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili)
Choir Type: Parish
Members: 3
WhatsApp Image 2025-09-01 at 21.16.17
01 September 2025
WhatsApp Image 2025-08-12 at 16.53.44
13 August 2025

Kwaya ya Mt. Sesilia ilianzishwa na kusimikwa rasmi mwezi August mwaka 1980 ikiwa na idadi ya wanakwaya 40 chini ya uongozi wa ndugu Melchior Haule. Kwaya ilianzishwa kuhudumia kigango cha Mavurunza ambacho kilikuwa chini ya parokia ya Msewe. Kigango cha Mavurunza hatimaye kilipandishwa hadhi ya kuwa parokia ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili mnamo tarehe 6Januari 2001. Kwaya ya Mt.Sesilia ni miongoni mwa kwaya zinazounda UKWAKATA katika dekania ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu Mavurunza.

Kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake, kwaya ya Mt. Sesilia imekuwa ikishiriki katika uinjilishaji kwa njia ya nyimbo na kuendeleza liturujia ya kanisa katoliki katika ibada mbalimbali. Tangu mwaka 2001 kwaya ya Mt. Sesilia imekuwa ikitoa huduma ya uimbaji kila domnika kwenye ibada ya misa ya 3 inayoanza saa nne kamili asubuhi.

Uongozi katika kwaya ya Mt. Sesilia katika vipindi mbalimbali tangu kuanzishwa kwake katika nafasi ya mwenyekiti ni kama ifuatavyo;

  • 1980-1983 || +MelchiorHaule
  • 1984-1986 || +PaulBwakila
  • 1987-1989 || +AidanNdunguru
  • 1990-1995 || +LucasZimamoto
  • 1996-1998 || +FrancisSakaya
  • 1999-2001 || +IsaacKilato
  • 2002-2006 || +AficanusMacnda
  • 2007-2009 || Boniface Mallya
  • 2010-2012 || +Africanus Maenda
  • 2013-2015 || Boniface Mallya
  • 2016-2019 || General Matembo
  • 2020-2022 || Cecilia Mtweve
  • 2023-2025 || Cecilia Mtweve

Idadi ya wanakwaya tangu kuanzishwa kwake imekuwa kati ya 40-50.

Kwa kipindi chote cha uhai wake, kwaya ya Mt. Sesilia imefanikiwa kurekodi albamu zifuatazo.

  • Machi 1997 - Nimeingia mahali patakatifu
  • Agosti 1998 - Enyi mumtafutao Mungu
  • Oktoba 2002 - Ee Mungu Baba Twakushukuru
  • Novemba 2005 - Nimefungua vitabu vyote,imeandikwa wapi? (audio)
  • Novemba 2006 - Nimefungua vitabu vyote, imeandikwa wapi? (video)
  • Oktoba 2012 - Nani aliye mkamilifu?
  • Julai 2016 - Sifa na Enzi (audio)
  • Disemba 2019 - Sifa na Enzi (video)

Mission:
Kumtumikia Mungu na Kanisa Katoliki kupitia nyimbo takatifu, kukuza mshikamano wa kiimani, na kuendeleza sanaa ya muziki wa liturujia kwa ustadi na ibada.

Activities & Ministries:
Kwaya huhudumu katika misa za Jumapili na Sikukuu za Kanisa, misa za ndoa, misa za jumuiya ndogo ndogo, na misa za kumbukumbu na shukrani. Pia hufanya mazoezi ya nyimbo mara kwa mara, kushiriki mashindano ya kwaya na matamasha ya kiroho, na kushiriki katika huduma za kijamii na upendo wa jirani.

LEADERSHIP
Choir Executive Committee
CM

CECILIA MTWEVE

Chairperson
AM

AGATHA MELEKI

Secretary
FM

FLORIAN MOSHI

Choir Master
MEMBERSHIP
Choir Members by Voice Parts

No choir member data is available at the moment.