Kwaya ya Mt. Anthony wa Padua ilianzishwa mwaka 1976, ikiwa na dhamira ya kuutangaza na kuusifu utukufu wa Mungu kupitia nyimbo na muziki wa Kanisa Katoliki. Mwaka 2026 kwaya hii itatimiza miaka 50 ya huduma ya uimbaji wa Injili na kuimarisha imani ya waamini.