Kwaya ya Mt. Fransisko wa Asiz (Kwaya B) ilianzishwa tarehe 04/10/1968 ikiwa ni kwaya maalum iliyotokana na mabruda wa kifransisko (Makapuchin).
Kwaya hii inahudumu katika misa ya pili kila dominika, kwa sasa tuna wanakwaya 51 ambao wanajitoa kwa hali na mali katika kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.