Kwaya ya Mt. Kizito Makuburi (KMK) ilianzishwa mwaka 1988 na ikapewa jina kwa heshima ya Mtakatifu Kizito (1872–1886), shahidi mdogo zaidi miongoni mwa Mashahidi wa Uganda. KMK ni kwaya ya Kanisa Katoliki kutoka Parokia ya Mwenyeheri Anuarite Makuburi, katika Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Dhamira kuu ya KMK ni kushiriki kikamilifu katika uongozi wa liturujia kupitia muziki mtakatifu, hususan katika maadhimisho ya Misa Takatifu, ili kuimarisha ibada na kuleta mshikamano wa waamini. Zaidi ya hapo, kwaya hii inajihusisha pia na shughuli mbalimbali za kijamii na kichungaji, zenye lengo la kujenga jamii yenye mshikamano, imani thabiti, na upendo wa kidugu, huku ikiutangaza mwili wa fumbo wa Kristo kupitia huduma ya muziki Mtakatifu. Kwa sasa, kwaya inaundwa na jumla ya wanakwaya 139.
Makuburi
Street.
Dar es salaam
Ilala
Tanzania
Simu: +255742000089
Barua Pepe: st.kizitochoir@gmail.com