Kwaya Mtakatifu Gabriel Malaika Mkuu Parokia ya Roho Mt Segerea Jimbo kuu la Dar es Salaam.
Ilianzishwa October 2009. Ikiwa na idadi ya WAIMBAJI kumi na nne baada ya kundi Moja lililokuwa likihudumia ibada mbili kugawana Katikati na kupata kwaya mbili zitakazo badilishana kuimba katika ibada .
Kwaya hizo zikiwa makundi mawili A na B
Kundi A.Baadae walipata jina lao baada ya kukaa pamoja na kujadiliana na kupendekeza jina ndipo walipopata jina la Mtakatifu Gabriel Malaika Mkuu (Nguvu ya Mungu)
Wanakwaya walivutiwa na jina hili baada ya ufafanuzi mzuri na maana ya Mt Gabriel Malaika Mkuu.Basi ndipo likaanza kutumika jina la Malaika Gabriel.
Kwaya hii imendelea na utume wake ndani ya Parokia,Ndani ya Jimbo Taifa na nchi za nje ikiwemo Kenya na nchi nyinginezo.
TUMEKUWA tukishiriki Matamasha mbalimbali ya Jimbo ndani ya nchi na nje ya nchi na Matamasha yenye viwango vya Kimataifa kama Tamasha la Yesu ni Mwema (TYM) zaidi ya mara tisa mfululizo pamoja na Tamasha la Holy Trinity nchini Kenya.
TUMEKUWA tukifanya utume wetu kadiri ya litrujia na Hiarakia inavyotuelekeza na kushirikiana na Mababa zetu Kwa Kila hatua.
Mission:
Kwaya inalenga kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji wa liturujia, kuwa chombo cha uinjilishaji kupitia sauti na muziki, na kueneza neno la Mungu ndani na nje ya parokia kwa kutumia vipaji vya waimbaji wake pamoja na teknolojia ya kisasa.
Sarah Johnson
David Kimani
Phone: +255 788 123456
Email: heavenlyvoices@example.com